Katika mahadhimisha hayo kulikuwa na mabango mbalimbali ya wafanyakazi yenye jumbe kwa kiongozi huyo wa nchi. Moja ya bango lilisomeka, 'Tupandishe Madaraja nasi tupande Bombardier'
Rais Magufuli aliliona bango hilo na kuamua kujibu kuhusu suala la kuwapandisha wafanyakazi madaraja.
"Kwenye mabango yenu nimeona moja ya bango limeandikwa 'Tupandishie Mishahara nasi tupande bombardier' imeandikwa kitaalam sana, nawapongeza sana"amesema.
Ameendelea kwa kusema,"Kuanzia mwaka 2015 tumewapandisha madaraja zaidi ya watumishi laki 1 na 18 elfu. Pia tumelipa madai yasiyo ya mishahara na mengi yalikuwepo kwa zaidi ya miaka 10,".
No comments:
Post a Comment