Baada ya kumaliza msimu kwa mafanikio, Simba leo itafanya tukio kubwa la kuwatuza nyota na wadau wake waliofanikisha mafanikio hayo katika tuzo zinazofahamika kama MO SIMBA AWARDS
Hafla ya tuzo hizo itafanyika kuanzia saa 12:30 jioni Kilimanjaro Hotel na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa Simba ambapo mgeni rasmi atakuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai
Tuzo hizo zilizoanzishwa mwaka jana, zimeingia kwenye msimu wa pili ambapo Simba itawatuza wachezaji walion'gara kupitia vipengele mbalimbali kama kipa bora, beki bora, kiungo bora, mshambuliaji bora na mchezaji bora wa msimu
Pia kutakuwa na tuzo kwa mchezaji chipukizi bila kusahau tuzo kwa mashambiki waliokuwa na mchango mkubwa katika uhamasishaji
Hafla hiyo itarushwa mbashara na Azam Tv kupitia Azam Sport 2

No comments:
Post a Comment