Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiiombea 'dua mbaya' Simba isishinde michezo yake na pengine wao kuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa
Msemaji wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki hao waache kuingilia kazi za waamuzi
"Ni jambo la ajabu kusema Simba imependelewa kisa mchezo kuongezwa dakika saba. Dakika hufidiwa pale mwamuzi anapoona muda ulipotezwa isivyo uwanjani," amesema Manara
Aidha Manara amewakumbusha mashabiki wa timu hiyo kuwa hata wao walipocheza na Lipuli Fc na kukubali kipigo cha bao 1-0 mkoani Iringa, waliongezwa dakika saba
Hesabu za Simba zimeendelea kukaa vizuri kuelekea ubingwa wa pili mfululizo baada ya ushindi wa Jana
Simba imefikisha alama 72 ikitofautiana na Yanga kwa alama tano tu huku mabingwa hao watetezi wakiwa na michezo mitano ya viporo
Simba iko katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wake
No comments:
Post a Comment