Chama wa wamiliki wa mabasi(TABOA)kimewataka wamiliki wote wa mabasi nchini kuanzia juni mosi kutopakia abiria wenye mizigo inawekwa katika mifuko ya plastiki ili kutekeleza agizo na makamu wa rais pamoja na sheria na kanuni za mazingira zinazoanza utekelezaji wake juni mosi mwaka huu.
Akizungumza katika kituo kikuu cha mabasi Ubungo,baada ya serikali kutoa agizo mweka hazina wa (TABOA) amewataka madereva na makonda kutekeleza agizo hilo na kudai (TABOA) hakitakubali kumtetea mmiliki yeyote atakaye kaidi agizo la serikali kwa kuuruhusu abiria wenye mizigo iliyoweka kwenye mifuko ya plastiki.
Baada ya jiji la Dar es Salaam kuwa la kwanza kutekeleza agizo hilo baadhi ya wananchi wameitaka zoezi la kuzuia mifuko ya plastiki kwenda sambamba na uwekaji wa vituo vya kukusanya mifuko hiyo katika mitaa ili kuiondoa katika mazingira.

No comments:
Post a Comment