Beki wa Kimataifa wa Uganda Juuko Murshidi amemaliza mkataba na klabu ya Simba na yuko mbioni kujiunga na moja ya timu za ligi kuu Afrika Kusini
Juuko aliyeitumikia Simba kwa misimu mitano, aliondoka mapema kwenye kikosi cha timu hiyo kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ya Uganda huko Arabuni
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitte, Juuko amethibitisha kuwa hataendelea kuitumikia Simba msimu ujao
"Napenda kuwashukuru kwa kipindi chote kizuri tulichokuwa pamoja. Ilikuwa ni safari nzuri kwani tulishirikiana pamoja ingawa wakati mwingine inatubidi kila mmoja kuwa mbali na wengine," aliandika Juuko
Juuko alikuwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba hasa katika michuano ya ligi ya mabingwa ambayo Simba iliondoshwa kwenye hatua ya robo fainali
Mwezi Disemba mwaka jana, Simba ilimuongezea mkataba wa miezi sita ambao unamalizika leo May 30

No comments:
Post a Comment