We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, May 1, 2019

Cannavaro alivyomuandaa mrithi wake 'Ninja'


Ukimfuatilia kwa umakini beki kisiki wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' huwezi kumtofautisha na aliyekuwa nahodha wa muda mrefu wa Yanga ambaye kwa sasa ni Meneja wa timu hiyo Nadir Haroub 'Cannavaro'
Licha ya kushabihiana kwa maumbile yao, wawili hao wanaotokea visiwani Zanzibar, wanashabihiana mpaka aina ya uchezaji wao

Baada ya kutundika 'daruga' mwishoni mwa msimu, viongozi wa Yanga walipanga kuistaafisha jezi namba 23 iliyokuwa ikitumiwa na Cannavaro ili kumpa heshima kutokana na utumishi wake wa kipekee wa zaidi ya miaka 12 katika klabu ya Yanga
Hata hivyo Cannavaro alipinga mpango huo, badala yake akaomba jezi hiyo atamkabidhi Ninja ili kumpa motisha akiamini beki huyo anaweza kabisa kuvaa viatu vyake


Jambo hilo halikuchukua muda mrefu kwani msimu huu Ninja amedhihirisha maono ya Cannavaro

Licha ya umri wake mdogo, Ninja amekuwa beki wa kutumainiwa katika kikosi cha Yanga huku kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera wakati mwingine akimtumia kama kiungo mkabaji 'kwa kazi maalum'
Mwenyewe Ninja amekiri kuwa Cannavaro amekuwa na mchango mkubwa kwenye mafanikio yake kwani alimsimamia tangu alipojiunga na Yanga mwaka 2017

"Cannavaro alikuwa zaidi ya nahodha na kaka kwangu," amesema
"Wakati naingia Yanga mwaka 2017, alinipa kipaumbele kwa kunielekeza mambo mbalimbali , Hakusita kunisahihisha pale nilipokosea na wakati wote alikuwa akinisisitizia niwe na nidhamu"

"Aliniambia kama nataka kufika mbali ni lazima niwe na nidhamu, nifuate maelekezo ninayopewa na nisikate tamaa"

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list