Mabosi wa TP Mazembe jioni hii watakutana na mama yake mzazi Ibrahimu Ajib kujadilia hatma ya mshambuliaji huyo aliyehaidiwa mshahara wa dola 5000 kwa mwezi akijiunga nao.
Pamoja na kuwepo kwa taarifa kuwa mabingwa hao wa Afrika mara tano, TP Mazembe wamefuta mpango wa kumsajili nyota huyo, lakini viongozi wa klabu hiyo wapo jijini Dar es Salaam kwa takribani wiki sasa kwa lengo la kumaliza usajili Ajibu.
Mmoja wa maofisa wa TP Mazembe amesema kocha wa TP Mazembe, Mihayo Kazembe na benchi lake la ufundi wanamtaka Ajibu na ndio maana wako Dar es Salaam hadi leo.
"Tangu tumefika hatujaonana na Ajibu isipokuwa ndugu yake tumeongea naye kwenye simu. Lengo ajiunge na TP Mazembe, lakini inavyoonekana kama hayuko tayari," alisema jamaa huyo.
"Tumeongea na kaka yake ametuhakikishia Ajibu hajasaini Simba, ametuambia tuonane na mama yake jioni hii na yeye atakuwepo, tunamsubiria.
"Kwa sasa alionekana tatizo linaonekana katika fedha pesa, yeye anataka nyingi zaidi ya ofa yetu TP Mazembe na wakati awali alikubali tena ilikuwa ndogo kabisa."
"Kwa sasa anasema anataka dola laki mmoja (zaidi ya Sh200 milioni) kwa sababu ndizo alizoahidiwa kupewa na mabosi wa Simba," alisema kiongozi huyo.Amesema, Mazembe wametoa ofa ya mshahara wa mwezi dola 5000 (zaidi ya Sh12 milioni) ameukubali. Tatizo fedha ya usajili dola elfu 50 (zaidi Sh120mil), lakini awali alikubali ndogo zaidi ya hii.
"Lakini, hii ameitaka sasa hivi kwa sababu awali tulikubaliana pesa ya usajili dola elfu thelathini na alikubali, lakini sasa amebadilika. Kwa hii dola elfu 50 ndio ametuambia tusubiri, tunamsikilizia."
Mmoja wa watu ambao wamekuwa wakimtumia na TP Mazembe kwa mambo mengi hata walipokuja kucheza na Simba, Patrick Kasangala alisema suala hilo ni kweli Ajibu amewaambia wasubiri.
"Jamaa wapo hapa wamepanga kuondoka kesho kama mambo yataendelea hivi. Wanasubiri kauli yake ya mwisho kwa sababu amewaambia wasubiri leo jioni," alisema Kasangala.

No comments:
Post a Comment