Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limemteua Mustapha Ghorbal wa Algeria kuchezesha mechi ya Robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na TP Mazembe.
Ghorbal atasaidiwa na Mahmoud Ahmed Kamel Abouelregal kutoka Misri na Mokrane Gourari kutoka Algeria pia
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, April 06 katika uwanja wa Taifa ukitarajiwa kuanza saa 10:00 Jioni.
No comments:
Post a Comment