Mwekezaji Mkuu wa Simba SC, Mohammed Dewji amesema kuwa suala la ujenzi wa Uwanja wao unafanyika Bunju jijini Dar es Salaam utakamilika mwezi ujao wa tano.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mo amesema tayari wameshamalizana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusiana na kuchukua nyasi zao bandarini pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
“Tumeshamalizana na mamlaka (TRA na TAKUKURU) hivyo uwanja upo chini yetu sasa. Tunangoja mvua zipungue baada ya wiki 2 tutaanza tena ujenzi. Mungu akijalia mpaka mwezi wa 5 uwanja wetu utakuwa umekamilika," amesema Mo.
No comments:
Post a Comment