We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, April 5, 2019

Uwanja mpya wa Tottenham washika nafsi ya pili kwa ukubwa London, Hazard aumwagia sifa “Wana uwanja nzuri hawajashinda taji kwa muda, sisi tumeshinda mara nyingi lakini hatuna”

Klabu ya Tottenham Hotspurs’ tayari imeufungua uwanja wake mpya ambao ulianza kujengwa mwaka 2016 ukiwa na uwezo wa kuingiza watu elfu 62062, Ukiwa ni uwanja wa pili katika jiji la London kuingiza watu wengi baada ya Wembley kuingiza watu elfu 90000. Uwanja wa Tottenham una urefu wa mita 105 na upana wa mita 68 sawa na yad (114.8 kwa 74.4).
Uwanja huu ukiwa umegharimu $ bilion 1.3 wakiupa jina la TOTTENHAM HOTSPUR STADIUM ambalo ni jina la muda kwani wanatarajia kulibadili jina hili Ingawa mashabiki wa timu hiyo wanapendekeza Uitwe “NEW WHITE HART LANE STADIUM”


Tottenham Hotspur ilijipatia rekodi iliovunja rekodi ya dunia ya £113m baada ya kodi msimu uliopita. Fedha hizo zimeshinda faida ya £106m ilizopata Liverpool mapema mwaka huu.


Matokeo ya kila mwaka ya kifedha ya msimu 2017-18 yanaonyesha kwamba mapato ya Spurs yalipanda kutoka £310m hadi £380m kutokana na mauzo ya wachezaji, mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Wembley na kufuzu katika awamu ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.


Takwimu hizo zilitolewa wakati ambapo klabu hiyo ilikuwa ikifungua uwanja wake mpya wa £1bn huku gharama hiyo ikiwa iliafikiwa kupitia mikopo.


Mapato yake katika ligi ya EPL yaliongezeka maradufu kutoka £19m hadi £42.6m kufuatia ongezeko la mshabiki katika uwanja wa Wembley. Tottenham iliishinda Crystal Palace 2-0 katika uwanja wao mpya.
“Nadhani Tottenham, kwa miaka miwili au mitatu, imekuwa moja ya timu bora nchini England. Hiyo ni kwa uhakika. Siipendi hiyo, kuwa wa haki – sisi ni Chelsea, na ni derby kubwa dhidi yao – lakini tunapaswa kukubali. Kwa Ligi Kuu ni nzuri: uwanja mpya, wana wachezaji wa juu. Lakini, mwishoni, unajua huko Chelsea tumeshinda nyara nyingi, na hawana. Kwa hivyo natumaini hii inaendelea. “

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list