Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewataka wabunge kuzifikisha fedha za maendeleo wanazopewa majimboni mwao.
Ameeleza hayo wakati Rais Magufuli yupo Mkoani Ruvuma ambapo anazindua barabara yenye urefu wa Kilometa 193 kuanzia Namtumbo-Kilimasera-Matemanga-Tunduru.
"Na nyie Wabunge mnapewa hela za majimbo ni zetu sote, wapo Wabunge wanapewa hizo hela wanakaa kimya, msikae nazo kimya, zisaidie kutatua kero za wananchi," amesema Rais Magufuli.
Ameendelea kwa kusema, 'Sisi ni Taifa moja michango ya maendeleo mengine Kilimanjaro, Mwanza, Mtwara tumeikusanya tukasema hii ni zamu ya Tunduru kupata barabara ya lami'
No comments:
Post a Comment