Mwekezaji Mkuu wa Simba SC, Mohammed Dewji amejibu tetesi zilizodai kuwa wachezaji wao, Meddie Kagere na Clatous Chama wanahitajika na baadhi ya vilabu vikubwa vya Afrika kutokana uwezo waliounesha kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Dar es Salaam, Mo Dewji amesema bado wanajenga timu na wachezaji hao bado wana mikataba.
"Ni kweli Simba tunahitaji pesa lakini tunahitaji ushindi na mafanikio kuliko pesa, kwa mwaka huu bonus tutakazotoa kwa wachezaji zitafika zaidi ya Billion 1"-Mohammed Dewji," amesema Mo Dewji.
"Mara nyingi unaweza kuona tumejaza uwanja lakini asilimia kubwa ya hizo pesa zinakwenda kwenye bonus za wachezaji kama tungefikiria pesa zaidi hizo bonus tungeshusha lakini sisi tunataka tuwape ari zaidi wachezaji wetu ili tupate mafanikio zaidi," ameeleza.
Mo amesisitiza kuwa, 'Kwa hiyo kwa hao wachezaji wawili mimi sio kocha lakini naimani kocha atataka kuendelea nao, kwa hiyo itakuwa ngumu kuwatoa Simba labda iwe kwa bei kubwa sana ili sisi tuweze kupata wachezaji wengine, hiyo itakuwa ni habari nyingine,'.
No comments:
Post a Comment