Shirika la umeme nchini, Tanesco, limetangaza msamaha wa riba kwa wateja wote wanaodaiwa na shirika hilo na kutoa mwezi mmoja kutakiwa walipe deni la msingi.
Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo ameeleza kuwa hadi sasa shirika hilo linadai zaidi ya shilingi bilioni 300 kutoka kwa wadaiwa wake na sasa wameamua kutoa msamaha kwa wadaiwa wote.
Chowo ametoa kauli hiyo kwenye maonyesho yaliyoandaliwa na Wakala wa Afya na Usalama mahala pa kazi (OSHA) yanayofanyika jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment