Leo mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wanashuka kunako uwanja wa Uhuru kuwakabili maafande wa JKT Tanzania katika mchezo ambao utapigwa saa kumi kamili jioni
Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika uwanja wa Taifa lakini umehamishwa ili kupisha ukarabati wa uwanja wa Taifa baada ya kumalizika mwa michuano ya AFCON U17
Simba inarejea uwanja wa Uhuru kwa mara ya kwanza msimu huu ikiwa na 'mfalme' Emmanuel Okwi ambaye msimu uliopita aliwea rekodi ya kupachika mabao mengi kwenye uwanja huo
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamedhamiria kushinda michezo yote iliyobaki, wanahitaji kushinda dhidi ya maafande
Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo ambao ulipigwa jijini Tanga, Simba iliondoka na ushindi wa mabao 2-0
No comments:
Post a Comment