Na: Theresia Mallya – Afisa Habari Tunduru DC
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa maagizo kwa waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 200 za kukamilisha ujenzi na upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera kilichopo Nakayaya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ametoa maagizo kwa waziri wa Tamisemi Mhe.Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 200 za kukamilisha ujenzi na upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera kilichopo Nakayaya wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.
Maagizo hayo ameyatoa wakati akitoa hotuba kwa wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko la Mchele –Nakayaya akiwa katika ziara ya kikazi siku ya pili mkoani Ruvuma.
Rais Magufuli alifikia uamuzi huo baada ya kuguswa na michango ya wananchi waliotoa katika kuchangia ujenzi wa kituo cha afya Juma Homera ya shilingi Milioni 189 ili kujenga kituo hicho kitakachosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru.
“Waziri wa Tamisemi nakuagiza ulete shilingi milioni 200 kwa ajili ya kufanya upanuzi wa kituo cha afya Juma Homera ili kitoe huduma za upasuaji,mionzi,kuongeza wodi za kutosha ili kurahisha huduma za afya kwa wananchi wa Tunduru”
Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli Alimuagiza waziri wa Tamisemi Selemani Jafo kutoa shilingi milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya katika Kata ya Namiungo ambayo haina zahanati wala kituo cha Afya katika vijiji saba vya kata hiyo.
Magufuli alilazimika kusimamisha msafara na kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamefunga barabara ambapo alisema kuna kila sababu ya kata hiyo kuwa na kituo bora na cha kisasa ili kupunguza vifo vya kinamama na wajawazito na watoto vinavyosababishwa na kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.
Hata hivyo alimaliza kwa kuwataka wananchi kufanya kazi na kushikamana katika kuijenga Tunduru na kuepuka chuki za kisiasa kwani maendeleo hayana chama, niwatake wanatunduru muungane kwa pamoja katika kuleta maendeleo chanya.
No comments:
Post a Comment