Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA, Patrick Ole Sosopi amelaani kitendo cha Jeshi la polisi kuendelea kufanya vitendo vya upendeleo na kutoweka usawa.
Sosopi ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Jeshi la polisi kuzuia kongamano la CHASO, UDSM, kwa madai kwamba taarifa za kiintelijensia kwamba hapatakuwa na usalama.
Sosopi ameeleza kwamba Polisi walianza kuzunguka eneo lilipokua likitarajiwa kufayika Kongamano hilo tangu saa 12 asubuhi.
"Nimezungumza na OCD wa Magomeni, sababu za kuzuia ni kwa Taarifa za kiintelijensia kwamba hapatakuwa na Usalama. Nalaani sana hiki kitendo cha polisi kuendelea kufanya Double standards", amesema Sosopi.
No comments:
Post a Comment