We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Saturday, April 6, 2019

Tetesi za usajili barani Ulaya Jumamosi hii, Hazard midomoni mwa Madrid, Bale, Pochettino, Lukaku, Rodri, Sancho na wengine sokoni

Mshambuliaji wa Chelsea mbelgiji Eden Hazard, 28,anajiandaa kutia saini mkataba wa kujiunga na Real Madrid siku chache zijazo. (Marca)Real Madrid inatafakari uwezekano wa kuwauza wachezaji wake Gareth Bale, 29, Toni Kroos, 29, na Isco 26. (Mail)



Hata hiyi Bale amejiondoa katika uwezekano wa kuhamia Manchester United, huku klabu hiyo ya ligi kuu ya England ikionekana kuelekeza darubini yake kwa Jadon Sancho, Callum Hudson-Odoi na Declan Rice. (Star)
Mkurugenzi mkuu wa AC Milan Ivan Gazidis, anamtaka meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino nafasi ya Gennaro Gattuso katika uwanja wa San Siro. (Corriere dello Sport – in Italian)


Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino (Katikati)
Image captionMeneja wa Tottenham Mauricio Pochettino (Katikati)

Tottenham wako tayari kutumia uero milioni 30 kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes, 25, ambaye yuko Barcelona kwa mkopo. (Telegraph)
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anapanga kufanya mazungumzo na nyota wa klabu hiyo Lionel Messi kurefusha mkataba wake katika klabu hiyo.
Mkataba wa Messi unakamilika mwaka 2021. (ESPN)


Lionel Messi
Image captionLionel Messi

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri hana uhakika ikiwa mkataba wa mkopo wa mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain 31, kutoka Juventus utageuzwa kuwa wa kudumu. (Guardian)
Mkurugenzi wa kiufundi wa Manchester City Txiki Begiristain alihudhuria mechi ya Atletico Madrid dhidi ya Girona siku ya Jumatano kufuatilia mchezo wa kiungo wa kati mhispania Rodri,22. (Mail)
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 25, atashauriana na klabu yake ya Manchester United kuhusu hatma yake katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu, kwa mujibu wa ajenti wake. (Sky Sports)


Romelu Lukaku
Image captionRomelu Lukaku

Chelsea ina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Atletico Paranaense Mbrazil Bruno Guimaraes, 21, msimu huu wa joto, licha ya marufuku ya usajili wa wachezaji waliyowekewa na shirikisho la soka Duniani Fifa. (ESPN)
Tottenham inatathmini uhamisho wa baadhi ya wachezaji wake akiwemo beki wa Uingereza Kieran Trippier, 28. (Evening Standard)
Mkurugenzi mkuu wa Borussia Dortmund amefutilia mbali uwezekano winga wa England Jadon Sancho, 19, kujiunga na Manchester United. (Metro)

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list