Mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na TP Mazembe umemalizika kwa sare ya bila kufungana katika Uwanja wa Taifa.
Mchezo wa Simba na TP Mazembe
Mchezo huo ambao ulikuwa ni wa kushambuliana katika dakika zote 90, umemalizika kwa sare huku Simba ikipoteza nafasi ya mkwaju wa penalti katika kipindi cha pili.
Katika dakika ya 59, Simba ilipata mkwaju wa penalti ambao nahodha John Bocco alikosa baada ya kupaisha juu.
Matokeo hayo ya sare, yanaifanya Simba kushindwa kuendeleza rekodi ya kushinda mchezo wa Klabu Bingwa katika Uwanja wake wa nyumbani. Mechi ya marudio itapigwa mjini Lubumbashi nchini Congo DR.
Matokeo ya mchezo mwingine, Al Ahly imefungwa mabao 5-0 na Mamelodi Sundowns katika mchezo uliopigwa nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment