Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa kiuongo wake Paul Pogba anayofuraha ndani ya klabu ya Manchester United licha ya ndoto za kijana huyo raia wa Ufaransa ni kutimkia Real Madrid ya nchini Hispania.

Pogba, ambaye mara kadhaa amehusishwa kutakiwa na klabu ya Madrid na Barcelona huko, amesikika akiizungumzia timu hiyo alipohojiwa kipindi alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa.
”Real Madrid ni ndoto za kila mtu, ni moja kati ya klabu kubwa duniani, Zidane ndiyo kocha pale kwa sasa, ni ndoto kwa kila mtoto na kila mchezaji,” amesema Paul Pogba.
”Kwa sasa ninayofuraha hapa Manchester, nina cheza nikiwa na kocha mpya. Kwa sasa nipo Manchester. Hatujui kitakachotokea baadaye.”
Hata hivyo kocha wa Real, Zinedine Zidane amewahi kusikika kuwa anavutiwa na Mfaransa mwenzake, Paul Pogba.
”Navutiwa kweli na Pogba na mnafahamu hilo, namfahamu mno, yeye ni mchezaji wa aina ya kipekee na mwenye umwezo wa kufanya vitu vingi kwasababu ya ujuzi na uwezo aliyonao. Anafahamu namna ya kushambulia na kujilinda, siku zote husema anaipenda Real Madrid,” amesema kocha huyo wa Real Madrid, Zinedine Zidane.
Hata hivyo kocha huyo wa Manchester, Solskjaer amesisitiza kuwa kijana huyo aliyeweka rekodi ya usajili ndani ya United kwa sasa ya pauni milioni 89 ataendelea kusalia Old Trafford kwakuwa anahitaji kuijenga upya.

”Nisingependa kuzungumzia wachezaji wa timu nyingine bila shaka lakini hii ni changamoto nyingine baada ya kutoka mapumziko. Wachezaji wamekuwa wakipatikana muda wote na mazingira tofauti,” amesema Solskjaer.
”Paul ni muelewa na heshima ambaye alimjibu maswali yake, Zidane ambaye ni ‘icon’ wa Ufaransa, kocha bora na mewahi kuwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa,” amesema Solskjaer.
Paulo ni mtu mzuri sana na mwenye heshima ambaye alijibu swali la jumla juu ya Zidane ambaye ni icon katika Ufaransa, meneja wa ajabu. Alikuwa mchezaji wa ajabu.
Bosi huyo wa United amethibitisha kuwa Romelu Lukaku na Anthony Martial watakuwa tayari kurejea uwanjani baada ya kuuguza majeraha.
No comments:
Post a Comment