Ndemla huyooo Yanga,Mwenyewe afunguka
Kiungo wa mabingwa wa soka nchini Said Ndemla hatimaye amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya uwepo wa tetesi nyingi zikimhusisha yeye kujiunga na Yanga ambao ni watani na wapinzani wakubwa wa Simba katika soka nchini Tanzania.
Said Ndemla amefunguka kuwa tayari washafanya mazungumzo ya awali na Yanga na wamemalizana kwenye mazungumzo hayo.
Amefunguka zaidi kwa kusema kiu yake yeye ni kuona anapata nafasi katika kikosi cha kwanza kitu ambacho amekuwa hakipati kwasasa ndani ya kikosi cha Simba.
Follow @Michezo_zone Instagram Bonyeza Hapa
” Yanga wameonesha nia ya kunisajili na maongezi ya awali tumemalizana . Uhakika wa namba kikosi cha kwanza ndio kiu yangu . Nadhani mambo yakienda sawa msimu mjao nitakuwa na timu hiyo . ”
Alisema Said Ndemla ambaye husifika zaidi kwa kupiga mashuti makali anapokuwa uwanjani.

No comments:
Post a Comment