We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, April 30, 2019

Mikononi mwa Polisi kwa kukutwa na nyaraka za serikali


Na Amiri kilagalila-Njombe

Kijana aliyefahamika kwa jina la Ford Abel Mwakatundu (28) mkazi wa makambako mkoani Njombe anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa makosa ya kukutwa na nyaraka za serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Salum Hamduni amesema kijana huyo anashikiliwa kwa makosa hayo kinyume na taratibu za kisheria.

"Mnamo April 22 mwaka huu majira ya saa 12:30 huko Makambako alikamatwa kwa kosa la kughushi nyaraka mbali mbali za serikali ikiwemo leseni za kuendesha magari,Tin number, Bima za magari pamoja na nyaraka za Sumatra zanazohusiana na Rout za mabasi na magari madogo ya biashara" alisema Hamduni

Ameongeza kuwa nyaraka hizo alikuwa akighushi na kuziuza kwa watu mbali mbali kwa kiasi cha Tsh 100,000 kwa lengo la kujipatia kipato. Kamanda amesema upelelezi unaendele na atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Meneja wa TRA mkoa wa Njombe, Musib shaaban ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia za kutumia njia za mkato kutafuta kipato kwa kuwa njia hizo zimekuwa zikikwamisha juhudi za serikali kuwaletea maendeleo. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list