KUBORESHA MAPENZI! NI Jumamosi nyingine tunakutana kupeana elimu ya mahusiano. Dunia ya sasa usipokubali kujifunza utapitwa na mengi.
Ni vyema kujifunza vitu vipya kila siku ili pia uhusiano wako uwe imara. Unapokubali kupitwa na wakati, maana yake hata kama huyo uliyenaye anakupenda sana, taratibu mapenzi yataanza kupungua na usipokuwa makini, huenda wajanja wakakuzidi akili na kukuacha ukilia na moyo wako.
Kama wewe na mwenzi wako mlikutana miaka ya nyuma ambapo hata simu hazikuwa zikitumika sana, kwamba kama ulikuwa ukihitaji kumuona ilikuwa ni lazime ukamsubiri chini ya mwembe au kichochoroni au umvizie akienda dukani, lazima uelewe kwamba zama hizo zimeshapita na wewe unatakiwa kulifanya penzi lako liendane na wakati. Nimewahi kukutana na kisa kimoja kwamba mume na mke walikuwa wakilumbana sana kisa kikiwa ni simu.
Kisa chao kinafurahisha sana, mke alikuwa akimlalamikia mume wake kwamba na yeye anataka anunuliwe simu ya kisasa (smartphone) kwa sababu mashoga zake wamekuwa wakimcheka kwamba yeye ni mshamba. Mume akawa hataki, anamwambia mkewe simu ya kazi gani wakati kila anapohitaji kuonana naye anamuona na kila siku wapo pamoja?
Akaenda mbali zaidi kwa kusema kuwa anang’ang’ania simu kwa sababu anataka awe anawasiliana na michepuko yake. Unaweza kuona kama ni suala dogo lakini ukilichunguza kwa makini, ni tatizo ambalo kama lisipopatiwa ufumbuzi mapema
Maoni ya mashabiki kuhusu mechi ya Azam vs Yanga SClinaweza kuja kuzaa tatizo lingine kubwa zaidi siku za baadaye. Maisha ya siku hizi, kama kipato kinakuruhusu, huwezi kuishi bila simu ya kisasa (smartphone) hata ya bei ndogo. Na kama mume unamiliki simu ya pesa kibao, kwa nini usimkumbuke na mwenzi wako? Ukisema uogope kumnunulia kwa sababu unahisi utakuwa unampa nafasi ya kukusaliti, mbona miaka ya nyuma simu hazikuwepo na bado usaliti ulikuwa ukitokea?
Kama mtu ana tabia ya usaliti, hata ufanye nini lazima atakusaliti tu, kwa hiyo hoja ya kushindwa kwenda na wakati wewe na mwenzi wako kwa kisingizio cha kuogopa kusalitiwa haina mashiko. Kuna raha yake ya kuwa na penzi linalokwenda na wakati, kwa mfano, unaweza kuwa unawasiliana na mwenzi wako kisasa kupitia WhatsApp au mitandao mingine ya kijamii.
Unaweza kumposti kwenye mitandao ya kijamii mwenzi wako huku ukimsindikizia ujumbe mzuri wa kumsifia, hii itafanya hata kama kuna watu wa pembeni walikuwa wakimnyemelea, wajue kwamba kumbe anaye mtu wake ambaye anampenda na kumjali.
Wanawake watakuwa mashahidi kwamba mara nyingi vitu vidogo huwa vinawafanya wajihisi kuwa na thamani ya kipekee mno, hebu jaribu kuposti picha yake akiwa amevaa mavazi mazuri ya heshima, akiwa amependeza na andika ujumbe wa kumsifia.
Huwezi kuamini utamfanya ajisikie raha sana ndani ya moyo wake, wanawake ni
mashahidi wa hili. Si hivyo tu, unaweza kumpeleka kwenye sehemu za kisasa za burudani, ambapo watu wanaokwenda na wakati hujumuika. Wanaume wengi, wapo radhi watoke out kwenda kwenye viwanja vya burudani na michepuko yao au marafiki, wakiwaacha wake zao nyumbani na watoto.
mashahidi wa hili. Si hivyo tu, unaweza kumpeleka kwenye sehemu za kisasa za burudani, ambapo watu wanaokwenda na wakati hujumuika. Wanaume wengi, wapo radhi watoke out kwenda kwenye viwanja vya burudani na michepuko yao au marafiki, wakiwaacha wake zao nyumbani na watoto.
Hii si sawa, mpeleke na yeye akaoshe macho, utalifanya penzi lenu liwe jipya na linalokwenda na wakati. Ukiona kitu kipya kimeingia, iwe ni fasheni ya nguo au kitu chochote na uwezo wa kumnunulia mwenzi wako unao, mfanyie sapraiz, siyo vitu vizuri vya kisasa avione kwa wenzake tu!
Yapo mambo mengi sana ya kujifunza kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi, acha kuishi naye kimazoea, hakikisha mnakwenda na wakati na hakika mtayafurahia maisha. Kwa leo ni hayo tu.
No comments:
Post a Comment