Hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuichangia Yanga iliyosimamiwa na Kamati Maalum iliyoundwa chini ya Mh Anthony Mavunde, ilifanyanyika kwa mafanikio makubwa Hotel ya Morena jijini Dodoma
Hafla hiyo iliyorushwa 'mbashara' na Azam Sport 2, iliwajumuisha wadau wa Yanga ambapo kupitia hafla hiyo fedha, ahadi na uhamasishaji mkubwa ulifanyika ili kuhakikisha Yanga inafikia lengo la kukusanya fedha za kutosha kwa ajili ya kukiboresha kikosi cha timu hiyo
Akifungua hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kamati Mh Mavunde alisema Kamati imeandaa mfumo mzuri wa kuwezesha upatikanaji wa fedha zitakazofanikisha mipango ya timu hiyo
"Lengo la kamati hii ni kuandaa mfumo mzuri utakaowezesha kupatikana pesa itakayofanikisha mipango ya timu yetu ikiwemo mwalimu kusajili wachezaji wazuri kwa msimu ujao," alisema
Mavunde aliwataja miongoni mwa wajumbe wa Kamati hiyo ambao anaamini kutokana na ushawishi wao katika jamii, wataweza kuharakakisha kukamilika kwa mpango huo
"Kamati yetu ina wajumbe takribani 28, na wengine ni watu wenye ushawishi katika maeneo mbalimbali.
"Lutawatangaza hapa kila mjumbe na mkoa atakaoratibu"
"Yupo Masoud Kipanya, Jokate Mwegelo, Said Ntimizi, Maulid Kitenge, Papaa Ndama na kipenzi cha wana Yanga Abdallah Bin Kleb na wengineo.
"Tumejipanga vema, wapenzi wa Yanga mna wajibu mkubwa wa kuinga mkono kamati hii ili kufikia malengo yaliyoanishwa"
Miongoni mwa wageni waliohudhuria hafla hiyo ni Mh Mwigulu Nchamba Rais wa klabu ya Singida United ambaye ni mdau mkubwa wa klabu ya Yanga
Nchemba ameahidi kusajili mchezaji mwingine kama alivyofanya kwa Feisal Salum na amemtaka kocha Mwinyi Zahera ampe jina la mchezaji mmoja miongoni mwa wachezaji nane wa kigeni ambao amepanga kuwasajili
"Kwa mara ya kwanza nimekaa na kuongea na Mwalimu wetu, hakika ana maono ya mbali na timu yetu," alisema
"Naahidi kuendelea kuichangia klabu yangu na naomba mwalimu anipe jina la mchezaji mmoja ntamsajili kama nilivyomsajili Fei Toto"
Wengine waliotoa ahadi kubwa ni pamoja na Mh Hussein Bashe ambaye ameahidi kutumia vyombo vyake vya habari kuitangaza bure kampeni ya kuichangia Yanga
Mh Bashe pia alichangia Fedha Taslim kiasi cha Tsh Milioni 10
Mdau mwingine wa Yanga Cyprian Musiba alichangia Mil moja huku pia akiahidi kuitangaza bure kampeni ya kuichangia katika vyombo vyake vya habari
Yanga huenda ikakusanya zaidi ya Mil 500 baada ya hafla ya jana kutokana na fedha taslim na ahadi zilizotolewa
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ni miongoni mwa wageni walioalikwa kwenye hafla hiyo
No comments:
Post a Comment