Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema, bado wana nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali licha ya kupata suluhu na TP Mazembe nyumbani kwa sababu inawezekana.
Kauli hiyo pia imeungwa mmkono na Kocha wa TP Mazembe, Mihayo Kazembe baada ya kutamka, hawawezi kushangilia mpaka watakaposhinda mechi hiyo ya marudiano itakayochezwa Aprili 13, Lubumbashi, DR Congo.
Aussems amezungumza hayo baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliochezwa leo Jumamosi Uwanja wa Taifa jIjinj Dar e Salaam.
"Nakubaliana na matokeo na kiwango walichoonyesha wachezaji wangu"
"TP Mazembe ni timu kubwa ingawa tulitakiwa kupata matokeo mazuri zaidi," alisema Aussems.
Amesema, walipata nafasi lakini walishindwa kufunga. "Nafasi zilikuwepo lakini ndiyo hivyo, sasa tunajiandaa na mechi ya marudiano tutafanikiwa tu,"alisema Aussems.
"Kupata sare nyumbani si kitu kizuri lazima utapata mshtuko kwa sababu tulitegemea kushinda." Kwa upande wa Kocha wa TP Mazembe, Mihayo Kazembe amesema, haukuwa mchezo rahisi na mashabiki wameshuhudia mchezo mzuri, sisi tulikosa bao na simba pia walikosa.
"Tunarudi Lubumbashi kwa maandalizi mengine na tunakwenda kujipanga na kuweka nguvu tushinde," alisema Mihayo. Kuhusu suluhu Mihayo amesema : " Hatuwezi kushangilia sasa kwa sababu ya matokeo ya suluhu tutafurahi baada ya mchezo wa mwisho watakapopata matokeo mazuri.
" Huo ni mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Simba na TP Mazembe, mechi ya marudiano itachezwa Lubumbashi, DR Congo.
Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment