Rais Dk. John Pombe Magufuli leo Aprili 30, 2019, alikuwa akiendelea na ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya na kusikiliza kero za wananchi wa mkoa huo, kukagua shughuli za maendeleo na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokamilika na ile inayotarajiwa kuanza kutekelezwa.
Akizungumza na wananchim mikoani humo, Magufuli ameonyesha kuchukizwa na makelele waliyokuwa wakipiga baadhi ya wananchi hao wakati yeye akiendelea kuzungumza hivyo kuamua kuwatolea uvivu kwa kuwataka waheshimu kile anachokizungumza kwani kina umhimu mkubwa kwao na Taifa kwa ujumla.
”Ifike mahali tuheshimu wale wengine na majibu yao, nimetumia muda huu hapa Tukuyu, bado kuna mikutano mingine inanisubiri… msinifanye kama mtoto mdogo….‘, alisema Magufuli akiwahimiza wananchi hao kutulia.
No comments:
Post a Comment