Jeshi la polisi Nchini limesema limejipanga vizuri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe,mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Simon Siro wakati akiwa katika ukaguzi wa kawaida, kukagua jeshi hilo pamoja vifaa mbali mbali kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa,amesema kuwa jeshi hilo limejipanga kikamilifu huku akiahidi kupambana na wachache watakao jaribu kuvuruga amani.
“Kwa uchaguzi huu wa serikali za mitaa tumejipanga vizuri sana kwa hiyo mtu asiwe na hofu lakini wale wachache watakaotaka kuleta vurugu huyo ni wa kwetu na wale waungwana tutakwenda nao vizuri kuhakikisha uchaguzi unakwenda vizuri mpaka ule wa 2020”alisema Siro
Aidha kamanda Siro amesema wakati wa uchaguzi kukiwa na amani huchaguliwa kiongozi mzuri huku kukiwa na vurugu hupatikana kiongozi wa hovyo, hivyo jeshi hilo na watanzania tunahitaji kiongozi mzuri ili kutufikisha mbele kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment