Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri Kangi Lugola amefanya ziara ya kushitukiza katika Kituo cha Polisi cha Sitakishari baada ya kuibuliwa kwa tuhuma za Askari Polisi kudaiwa kuwafanyia vitendo vya Ulawiti watuhumiwa wanaofikishwa kituoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kangi Lugola amesema nchi ni kubwa na ina mikoa na wilaya nyingi za Kipolisi ambapo akiwa katika Bunge la Bajeti Dodoma moja ya jambo lililoibuka kutoka kwa Wabunge ni kwamba kuna baadhi ya vituo vya Polisi ikiwemo Sitakishari, askari wanatuhumiwa kulawiti watuhumiwa.
“Kama waziri lilinishtua na sitarajii lifanyike katika vituo vya Polisi, hivyo nikaja hapa nikaonana na Mkuu wa Polisi Ilala, Mkuu wa Polisi wa wilaya na Naibu Upelelezi wa mkoa nimezungumza na kuwapa maelezo wafanya uchunguzi na kama yapo yafanyike maamuzi,“amesema.
No comments:
Post a Comment