We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, March 4, 2019

Zahera awafungukia Simba hawana uwezo wa kumsajili mchezaji kutoka AS Vita


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema kuwa Klabu ya Simba hawana uwezo wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya AS Vita Club, Jaen Mark Makusu. 

Imeelezwa kuwa Zahera amewaeleza Simba hawatakuwa na uwezo wa kumlipa mchezaji huyo kwani kiwango cha malipo yake wao hawajawahi kukifanya kwa mchezaji yoyote yule. 

Ameeleza Makusu amekuwa akilipwa kiasi cha mshahara wa milioni 39 kwa mwezi wakati Simba inatajwa mchezaji anayelipwa fedha ya juu ni Emmanuel Okwi anayepokea milioni 12. 

Kauli ya Zahera imekuja kufuatia uwepo wa tetesi kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumsajili Makusu ambaye yupo na VIta inayoshuka dimbani Jumamosi ya wiki hii kucheza na Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Simba imetajwa kutaka saini ya mchezaji huyo ambaye wanaamini atawasaidia zaidi kwenye michezo ya kimataifa na hata Ligi Kuu Bara haswa kuiboresha safu ya ushambuliaji. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list