We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, March 25, 2019

Vigogo 3 wa CCM, wakamatwa wakipokea rushwa ya milioni 5

Viongozi wa tatu wa Chama Cha Mapinduzi wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kutokana na kosa la kuomba milioni tano za rushwa kwa mwananchi aliyekuwa akitaka kupanga katika viwanja vya CCM.

Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Ilala Christopher Myava,  amesema kwamba Takukuru Ilala ilipokea taarifa Machi 22, kutoka kwa raia huyo aliyeombwa rushwa.

Viongozi hao wametajwa kuwa ni Jenipha Mushi Katibu wa CCM tawi la Amana, Ilala, Katibu Kata ilala, na Frank Mang'ati ambaye ni Katibu wa Hamasa Dar es salaam.

Amesema kwamba walitengeneza mtego baada ya kupewa taarifa ambapo mshtakiwa wa kwanza alikamatwa eneo la Msimbazi Sekondari akiwa na kiasi ch sh.milioni tatu huku wenzake wakiwa wanamsubiri katika eneo la klabu ya wazee kwa ajili ya mgao wa pesa.

"Miradi mingi ya CCM ambayo baadhi ya wanachama wasiokuwa waaminifu, wamekuwa wakiitumia vibaya, sasa nitoe wito kwao kwamba TAKUKURU haitosita kuwachukulia hatua za kisheria" - amesema Christopher Myava.

Ameongeza kwamba mapambano ya kupambana na rushwa yanatengemea sana taaarifa za wananchi hivyo wananchi wasiwe kimya wanapokutana na changamoto ya kushawishiwa kutoa taarifa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list