We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

Vibaka Wavamia Wodi Ya Wagonjwa katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi

Watu wawili wanaodaiwa kuwa vibaka, wamevamia kwenye wodi namba moja katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu.

Watu hao ambao inadaiwa walikuwa wawili, waliingia katika hospitali hiyo jana alfajiri Machi 25, 2019 majira ya saa 10:00 na kuiba vitu hivyo ambavyo ni mali za wagonjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai watu hao wawili ni vibaka.

Akizungumza shuhuda wa tukio hilo, Rebeca Msigiti ambaye alikuwa msaidizi wa mgonjwa katika wodi hiyo, amesema watu hao ambao ni wanaume, waliingia wawili ambapo mmoja alibaki mlangoni na mwingine akaingia ndani na kuchukua simu za wagonjwa na mikoba yao.

Amesema watu hao walipoingia wodini wao walidhani ni madaktari wameingia, kumsaidia mgonjwa ambaye alikuwa amezidiwa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list