Timu ya Taifa ya Burundi jana iliandika historia ya kukata tiketi ya kushiriki fainali za AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya kutoka sare ya ao 1-1 dhidi ya Togo matokeo ambayo yamewapa nafasi ya kwenda Misri
Burundi imeungana na Uganda na Kenya kuwa timu kutoka Afrika Mashariki ambazo zimefuzu kwa fainali hizo zitakazopigwa mwezi Juni mwaka huu
Leo Tanzania inaweza kuwa timu ya nne kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kufuzu kwa fainali za michuano hiyo kama itapata ushindi dhidi ya Uganda huku ikiomba matokeo mabaya kwa Lesotho
Ni mchezo wa 'kufa au kupona' kwa Stars ambayo inajaribu kurudia kile ilichokifanya miaka 39 iliyopita kwa kutinga fainali za michuano hiyo zilizofanyika Nigeria mwaka 1980
Mchezo dhidi ya Uganda utapigwa saa 12 jioni sambamba na mchezo mwingine wa kundi L kati ya Cape Verde dhidi ya Lesotho
Kila la kheri Stars...!

No comments:
Post a Comment