We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

TFF yazungumzia Kapombe kupata zawadi ya JPM

Uongozi wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF umezungumzia juu ya uwezekano wa mlinzi wa klabu ya Simba na Taifa Stars, Shomari Kapombe kujumuishwa katika zawadi iliyotolewa na Rais Magufuli kwa wachezaji wa Taifa Stars.
Shomari Kapombe ( kushoto ) na Rais Magufuli (kulia) akisalimiana na wachezaji.
Kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Wilfred Kidau, TFF imesema kuwa suala la Kapombe kuhusika katika zawadi ya viwanja iliyotolewa na Rais Magufuli haliko mikononi mwao, bali lipo katika Ofisi ya Rais chini ya wasaidizi wake.
Amesema kuwa Ofisi ya Rais ndio wanafahamu ni wachezaji wangapi na namna gani ya kutoa zawadi hiyo, na kwamba wao TFF hawana mamlaka ya kuingilia mipango yao bali wanasubiri maelekezo.
Jana Jumatatu, Machi 25, Rais Magufuli alikutana na wachezaji wa Taifa Stars, Kamati ya Uhamasishaji ya timu ya Taifa pamoja na Bondia Hassani Mwakinyo ikiwa ni siku moja baada ya timu hiyo kufuzu michuano ya Mataifa Afrika AFCON 2019, yatakayofanyika nchini Misri mwezi Juni hadi Julai.
Ikumbukwe kuwa Shomari Kapombe alipata majeraha akiwa katika kambi ya Taifa Stars nchini Afrika ya Kusini, wakati wa maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Mataifa y afrika AFCON dhidi ya Lesotho, mchezo ambao Taifa Stars ilipoteza kwa bao 1-0 ugenini mwezi Novemba mwaka 2018.
TFF, Kapombe akiwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi
Bonyeza hapa chini kutazama zaidi Katibu Mkuu wa TFF akizungumza.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list