Bodi ya Ligi Kuu imetangaza kuitoza klabu ya Yanga faini ya Tsh Milioni Sita kutoka na makosa yaliyofanyika katika mchezo dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa Taifa
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema Yanga imetozwa fainali ya Tsh Milioni 3 kwa kila kosa kutokana na makosa mawili iliyofanya kwenye mchezo huo
Makosa hayo ni kuingia uwanja bila kupitia mlango rasmi na kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mapumziko
No comments:
Post a Comment