Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy angetaka £130m kutoka Real Madrid kwa ajili ya mchezaji wa safu ya kati wa Denmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27. (Sunday Mirror)
Wakala wa mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United Paul Pogba , Mino Raiola, amezungumzo mara mbili kwa simu na Real juu ya kuhamia kwa mchezaji huo mwenye umri wa miaka 26 Uhispania . (Marca, via Manchester Evening News)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amemuambia Pogba kuwa namtaka katika Bernabeu na akasisitiza kuwa hajui ni kwanini mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa asingependa kuhamia Katika timu hiyo. (Sunday Mirror)
Paris St-Germain watatimiza kiwango cha David de Gea cha kumnunua kwa £350,000 katika kipindi cha wiki moja na mlinda lango huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28 ataelekea Manchester United kama watashindwa kumlipa kiwango hicho. (Sun on Sunday)
Real Madrid bado wanatathimini iliwa watajiunga na PSG kujaribu kusaini mkataba na in De Gea, huku klabu ya Italia ya Juventus pia ikitathmini hilo . (Sunday Express)
Chelsea hawana mpango wa kufanya mazungumzo na winga Callum Hudson-Odoihadi msimu ujao, wakati mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingerexza mwenye umri wa miaka 18 atakapokuwa amebakiza mwaka mmoja wa mkataba wake. (Mail on Sunday)
Meneja wa Blues Maurizio Sarri ni chaguo la kwanza la Romakuwa meneja wao msimu ujao. Meneja wa zamani wa Chelsea na Leicester Claudio Ranieri ndiye anayeongoza upande wa timu za kundi A zilizofuzu katika Uefa championi, kwa kuteuliwa kuendelea kuiongoza timu hiyo hadi mwishoni mwa msimu huu kufuatia kufutwa kazi kwa Eusebio di Francesco. (Sunday Express)
Atletico Madrid na Barcelona wanamtaka mchezaji wa safu ya kushoto nyuma wa timu ya England Leicester City -Ben Chilwell, mwenye umri wa miaka 22, kwa £50m. (Sun on Sunday)
Manchester United watatia zaidi mkazo juu ya sera yao ya kuhama inayowahusu wachezaji wenye umri mdogo , huku mchezaji wa safu ya kati wa timu ya Crystal Palace ya England ya wenye chini ya umri wa miaka -21 anayecheza safu ya kulia nyuma Aaron Wan-Bissaka,mwenye umri wa miaka 21, akiwa mmoja wa walengwa . (Mail on Sunday)
Inter Milan wamekubali kuongeza mara dufu mshahara wa Milan Skriniar, mwenye umri wa miaka 24, ili kumzuwia mlinzi huyo wa Slovakia kuhamia katika moja ya wenyeji wa klabu za Ligi ya Primia, wakiwemo Manchester United, Liverpool, Chelsea na Manchester City. (Sunday Mirror)
Leicester wanakamilisha mkataba wa £40m kwa ajili ya deni la mchezaji wa kiungo cha kati wa Monaco Youri Tielemans, huku kukiwa na fununu kwamba Tottenham na Manchester United wanataka kumchuku kijana huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 21. (Sun on Sunday)
Mchezaji wa safu ya kati wa timu ya England ya West Ham Declan Rice, mwenye umri wa miaka 20, amepuuza madai ya kwamba anataka kuhama kwenye hiyomsimu huu, baada ya kuhusishwa na Manchester City. (BT Sport, via Manchester Evening News)
Mshambuliaji wa Scotland anayeichezea West Brom kwa deni Oliver Burke, mwenye umri wa miaka 21, anasema atafurahia sana iwapo atapata fursa ya kubakia Celtic. (Daily Record)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane anasisitiza kuwa mlinzi Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25, ni mwenye furaha katik aklabu hiyo , licha ya tetesi kwamba mfaransa huyo anataka kuhamia United. (Manchester Evening News)
Mchezaji wa Liverpool Muhispani Pedro Chirivella mwenye umri wa miaka 21 ambaye anachezea timu ya Extremadura kwa deni hadi mwisho wa msimu ambaye hawezi kucheza baada ya kushindwa kutoa tarehe ya mwisho , anataka kurejea Uhispania Muhula ujao . (Liverpool Echo)
Mlinzi wa Ajax Mholanzi Matthijs de Ligt anasema anaweza kusaini mkataba na Juventus, huku Liverpool na Arsenal wakionyesha nia ya kumtaka. (Talksport)
Barcelona wako tayari kumsikiliza Mkroasia Ivan Rakitic mwenye umri wa miaka 31 anayechezea safu ya kati juu ya juu ya pendekezo lake la malipo ya £40m , wakati Manchester United nao wakimsaka . (Mundo Deportivo)
Meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo amepuuzilia mbali taarifa zozote zinazosema kuwa anaweza kuhamia Chelsea. (Metro)
No comments:
Post a Comment