Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amesema kikosi cha timu hiyo kimepania kushinda mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Alliance Fc utakaopigwa March 30 katika dimba la CCM Kirumba
Ten amesema Yanga imekuwa ikijifua katika uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam chini ya kocha Msaidizi Noel Mwandila ambaye ameachiwa program za mazoezi na kocha Mwinyi Zahera
Amesema baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi kuelekea mchezo huo na anaamini mpaka siku ambayo kikosi kitaelekea Mwanza wachezaji wote watakuwa 'fit' kuikabili Alliance Fc
"Mchezo dhidi ya Alliance Fc tunauchukulia kwa umuhimu mkubwa kwani tukitwaa ubingwa wa FA tutajihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao," amesema Ten
"Hivyo hatuwezi tukaacha nafasi hiyo ipite kirahisi"
Juma Mahadhi na Raphael Daudi ni miongoni mwa wachezaji walioanza mazoezi ambao walikuwa nje kwa muda mrefu
TAFADHALI TUNAOMBA UTUPE NYOTA 5 KWA KU RATE APP YETU CHINI YA RADIO
No comments:
Post a Comment