Kiungo wa Kagera Sugar, Behewa Sembwana amefariki dunia leo alfajiri kutokana na kuugua tumbo.
Kiungo huyo amesumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa muda mrefu, hali ambayo ilimlazimu kufanyiwa operesheni takribani mara mbili.
Nahodha wa timu hiyo, George Kavila amethibitisha kuwa Behewa amefariki baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo ambayo alianza kulalamika tangu wakiwa pamoja kikosini.
“Nakumbuka alianza kuumwa wakati tunacheza na Mwadui, alishindwa kutoka na sisi kwenda kule Complex baada ya hapo alipelekwa hospitali alipatiwa matibabu, lakini baadaye alihamishiwa Muhimbili ndio mauti yakamkuta akiwa hapo,” alisema Kavila.
Aliongeza kwamba mchezaji huyo ameondoka akiwa na umri mdogo licha na alikuwa amebarikiwa kipaji hasa katika kuuchezea mpira anapokuwa yupo uwanjani.

No comments:
Post a Comment