Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumapili kinashuka kwenye uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga kuikabili Stand United kwenye mchezo wa ligi raundi ya 29
Simba iko Shinyanga tangu juzi ikijiandaa na mchezo huo unaotarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi kamili jioni
Mabingwa hao watetezi wameahidi kuendeleza moto wa ushindi mfululizo kwenye ligi wakiwa wametoka kushinda michezo yote mitano iliyopita
Katika mchezo wa leo Simba itamkosa mshamuliaji wake Emmanuel Okwi ambaye anauguza majeraha aliyopata kwenye michezo dhidi ya Azam Fc na Lipuli
Hata hivyo leo huenda kiraka Erasto Nyoni akarejea kikosini baada ya kupona majeraha ya goti yaliyokuwa yakimsumbua
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamefuata alama tatu mkoani Shinyanga na watahakikisha wanalikamilisha hilo
Ushindi kwenye mchezo wa leo utaifanya Simba ifikishe alama 51 na kuendelea kukaribia kuipiku Azam Fc yenye alama 53 katika nafasi ya pili
No comments:
Post a Comment