We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, March 1, 2019

Shirika la UNFPA lapongezwa kwa ujenzi wa jengo la upasuaji Kituo cha Afya Nassa



Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani (UNFPA) limepongezwa kwa ujenzi wa jengo la upasuaji na wodi ya mama na motto katika kituo cha Afya Nassa kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

Pongezi hizo zilitolewa jana na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Dkt Godfrey Mbangali mbele ya Mratibu wa shirika la UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Dinah Atinda mara baada ya kutembelea majengo mapya ya upasuaji na wodi ya mama na motto katika kituo hicho.

Aliongeza kuwa kuwepo kwa majengo hayo kumesaidia sana katika kuboresha huduma katika eneo hilo na hivyo kuondokana na mtindo wa kuwa na wagonjwa waliokuwa wakirundikana sehemu moja na sasa wamepata fursa ya kupata huduma ya upasuaji.

Dkt Mbangali alisema kuwa kukamilika kwa majengo hayo kumewezesha kuanzishwa kwa huduma za upasuaji katika kituo hicho cha afya na hivyo kuwapunguzia adha ya kwenda kufuata huduma za upasuaji kwa wakazi wa wilaya hiyo wapatao 203,597 katika Hospitali teule ya Bariadi na Hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Aliongeza kuwa kabla ya kuanzishwa kwa huduma za upasuaji kituoni Nassa mgonjwa alilazimika kupewa rufaa kwenda Hospitali teule ya Bariadi na kisha alitakiwa kupelekwa Bugando mwanza kama angehitajika kupata rufaa zaidi.

“Ukiangalia jiografia ya jimbo la Busega ambalo linapakana na mkoa wa mwanza mgonjwa angelazimika kuzunguka kwanza kwenda Bariadi na kisha kupelekwa Bugando Mwanza, ambapo ni mzunguko mrefu,” alisema.

Kulingana na mazingira ya kijiografia ya wilaya ya Busega, kama kusingekuwa na huduma ya upasuaji, mgonjwa kwanza angelazimika kwenda Bariadi na kama angezidiwa zaidi angelazimika kupelekwa jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Dkt Mbangali aliongeza kuwa mbali na wilaya hiyo kuwa na vituo vya afya vinne lakini ni kituo cha Nassa pekee ndicho kinachotoa huduma za upasuaji wilayani humo.

Aliongeza kuwa tangu huduma za upasuaji zianze kituoni hapo, jumla ya wagonjwa 12 wamekwishafanyiwa upasuaji wilayani humo na wote wanaendelea vizuri baada ya kupata huduma hizo.

Mbali na ujenzi wa jengo, UNFPA pia walitoa vifaa mbalimbali vinavyohitajika maabara kama vile vitanda, mashine ya usingizi pamoja na mashine ya kufyonza damu ili sehemu iliyofanyiwa huduma za upasuaji iweze kupona kwa haraka.

Naye Mratibu wa UNFPA kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bi Dinah Atinda alisema kuwa kituo cha Nassa ni miongoni mwa vituo na zahanati 38 kutoka mkoa wa Simiyu ambazo zilipata fedha za ujenzi wa majengo ya wodi ya wazazi na jengo la upasuaji ambapo kituo hicho kilipokea jumla ya shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo ya mama na mtoto na jengo la upasuaji na shilingi milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mingine katika kituo hicho ukiwemo ujenzi wa jengo la maabara.

Pia Bi Atinda aliusifu uongozi wa wilaya ya Busega kwa kuweza kusimamia kikamilifu fedha za serikali katika ujenzi wa majengo hayo mawili.

Mbali na Kituo cha Afya Nassa, UNFPA walifadhili ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika zahanati za Kiloleli, Badugu, Igalukilo, Ngasamo na Nyamikoma

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list