Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo, amesema kuwa Serikali imewapa fursa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano kubadili tahsusi na kuchagua wanachokitaka kukisomea.
Hayo ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa hiyo ya wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha tano kwa waandishi wa habari jijini Dodoma.
Waziri Jafo amesema kuwa hali hiyo inatokana na baadhi ya wanafunzi ambao hawakujaza vizuri tahasusi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu.
Jafo amesema ofisi yake haitatoa fursa ya mwanafunzi yeyote kubadili tahasusi anayotaka kama asipotumia fursa hiyo.

No comments:
Post a Comment