Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara kuanzia April 2 hadi 4, 2019 .
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema katika ziara hiyo Rais Magufuli atazindua na kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema ataweka jiwe la msingi upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara, barabara ya Mtwara-Mnivata, kiwanda cha kubangua korosho na katika chuo cha ualimu cha Kitangali wilayani Newala.
Aidha amesema Rais Magufuli atazindua kituo cha afya cha Mbonde wilayani Masasi na barabara ya Mangaka-Mtambaswala na Mangaka -Nakapanya iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
“Ni miradi mikubwa ambayo itasaidia kuchochea kukua kwa uchumi wa Mtwara na nchi kwa ujumla, ni miradi ambayo kwa Mtwara ina tija kubwa sana kwa hiyo niwaombe wananchi wajitokeze kwa wingi katika maeneo yote yenye miradi ya maendeleo kuja kumsikiliza kiongozi wetu wa kitaifa ambaye ni mtetezi wa wanyonge,” amesema Byakanwa
No comments:
Post a Comment