Rais John Magufuli ametoa ndege moja ya serikali kwa ajili ya kuusafirisha mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utakaopelekwa Bukoba kwa maziko.
Msemaji wa familia, Raymond Kashasha amesema hayo leo Machi 1, 2019 alipozungumza na waandishi wa habari..
Ruge anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatatu kijijini kwao Kiziru wilayani Bukoba mkoani Kagera na atasafirishwa kutokea Dar es Salaam siku ya Jumapili, Machi 3.
No comments:
Post a Comment