We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, March 3, 2019

Polepole: Kanuni daima zitabaki kuwa kanuni na hazitabadilika


Baada ya Chama Cha Mapinduzi kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA kwa mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa mwishoni mwa wiki hii, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole amesema si kwa sababu ya nafasi ya kugombea.

Akijibu maswali pamoja na maoni ya wafuasi wake katika ukurasa wake wa twitter, Polepole amesema kwamba Chama hicho kitaendelea kusimamia kanuni na kuwa hazitabadilika.

''Kanuni daima zitabaki kuwa kanuni na hazitabadilika, lakini wakati huu hali ni tofauti , Hatutaki mgombea wa urais. Mtu ameomba nafasi ya uanachama, we are a mass party but very keen as to who becomes our leader jana, leo na kesho!".

Hivi karibuni Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa urais mwaka 2015 kupitia UKAWA, alitimkia CCM huku akisema kwamba amerejea nyumbani. 

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list