We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, March 25, 2019

NEC ilivyojipanga kumaliza malalamiko


Ushirikishwaji wa vyama vya siasa na wadau mbalimbali wa uchaguzi katika shughuli za kiutendaji za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) umekuwa ajenda inayoibuliwa kila wakati Tume inapokuwa inatekeleza majukumu yake. 

Kwa nyakati tofauti baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wamenukuliwa wakilalamika kupitia kwenye vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuelezea kinachodaiwa kwamba ni ukosefu wa ushirikishwaji wa moja kwa moja katika utekelezaji wa majukumu ya tume (NEC). 

Ajenda ya vyama vya siasa inajengeka juu ya ukweli kwamba, wao ndio wadau wakuu katika utekelezaji wa majukumu ya NEC kama yalivyoainishwa katika Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. 

Majukumu hayo ni pamoja na kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapiga kura katika uchaguzi wa Rais na wabunge katika Jamhuri ya Muungano, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa uchaguzi wa rais na wabunge, kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge. 

Majukumu mengine ni pamoja na kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapigakura na uendeshaji wa uchaguzi wa madiwani wa Tanzania Bara na kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliokusudia kuwashirikisha kwenye maboresho ya kanuni zinazohusika na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura, Mwenyekiti wa NEC hivi karibuni, Jaji Semistocles Kaijage anasema NEC itadumisha utaratibu wa kuwashirikisha wadau wake katika kila hatua ya utekelezaji wa majukumu yake. 

Licha ya kusisitiza kwamba hakuna sheria yoyote inayoilazimu Tume kuwashirikisha wadau wake, Jaji Kaijage anasema Tume itaendeleza utamaduni huo ili kujenga uhusiano mwema na ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake. 

"Sasa hivi tunapokwenda kutakuwa na mabadiliko ya mambo mbalimbali kwa hiyo tutajitahidi kuyawasilisha kwa wakati na ndiyo maana hata uboreshaji hatutafanya kabla hatujakutana na nyie (vyama vya siasa) na hiyo ni kwa kila hatua,"alisema Kaijage. 

Anaongeza kuwa, hatua ya kwanza kabisa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 ni kupitia kanuni zitakazoongoza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura. 

Mwenyekiti huyo anasema "Kanuni zikishaeleweka kwa wadau na wananchi kwa jumla, zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura litakwenda kwa urahisi na ndiyo maana tumejipanga kuwashirikisha wadau wetu wote katika kila hatua kabla ya Uchaguzi Mkuu." 

Anataja baadhi ya wadau muhimu kwamba ni pamoja na waandishi wa habari, vyama vya siasa, asasi za kiraia na asasi za kidini na kuongeza kwamba, mambo yote ya maandalizi ikiwa ni pamoja na manunuzi ya vifaa yatazingatiwa ili kuhakikisha kwamba, hatua zote kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 zinafanikiwa. 

Kwa mujibu wa Kifungu cha 15(5) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 21(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura ya 292, Tume inapaswa kuboresha Daftari la Kudumu la Wapigakura mara mbili katika Uchaguzi Mkuu mmoja na Uchaguzi Mkuu mwingine unaofuatia. 


"Pamoja na kupewa mamlaka hayo kisheria, Tume imejiwekea utaratibu wa kuwashirikisha wadau katika shughuli mbalimbali za kiuchaguzi, ili kuhakikisha inajenga na kutekeleza misingi ya kidemokrasia katika kusimamia, kuratibu na kuendesha uchaguzi zilio huru, wazi, wa haki na wa kuaminika," alisema Kaijage. 

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athumani Kihamia anasema mabadiliko hayo ya marekebisho ya kanuni hayana athari katika taratibu, sifa na masharti ya kujiandikisha kuwa mpiga kura. 

Kihamia anasema kimsingi, maboresho yamehusisha mambo kadhaa kama vile kutoa tafsiri ya baadhi ya maneno ambayo hayakuwa yametafsiriwa, kupanga upya kanuni na kubainisha majukumu ya watendaji wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura. 

Mengine ni pamoja na kusahihisha makosa ya kisarufi na kimantiki, kuboresha fomu zinazotumika katika zoezi la uandikishaji na kuainisha sifa za mtu kuandikishwa. 

Akizungumzia ushirikishaji wa wadau Dk Kihamia anasema katika kutekeleza misingi ya kidemokrasia na uendeshaji wa uchaguzi ulio huru, wazi na wa haki, NEC imejiwekea utaratibu wa kushirikisha wadau katika shughuli mbalimbali za kiuchaguzi. 

Tunataka kuendesha Tume ya kisasa na ya kisayansi kwa maana ya kuwashirikisha wadau ambao wahusika wakuu ni vyama vya siasa na tunafarijika kwamba, wengi wanaohudhuria ni viongozi waandamizi, tunafanya hivi kwa sababu tunataka twende pamoja, tuamue pamoja na kuepusha malalamiko

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list