We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ameeleza msimamo wake kuhusiana na Shomari Kapombe ambaye aliumia mwaka jana akiwa katika majukumu ya Taifa Stars, RC Paul Makonda ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars aliahidi Tsh milioni 10 kwa kila mchezaji kama wataiwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 2019.

Shomari Kapombe
Sasa baada ya zawadi hiyo kutoka na wachezaji kupewa viwanja na Rais Magufulikama sehemu ya zawadi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 2019 kwa kuifungaUganda 3-0, Samatta ameamua kuwakumbusha shirikisho la soka Tanzania TFF kuwa Shomari Kapombe anatakiwa kukumbukwa katika mgao huo.
“Shomari kapombe kama captain ningeomba TFF imuangalie katika zawadi ambazo wachezaji watapata, ikishindikana basi ningeomba wachezaji wote tumchangie kidogo kidogo na endapo vyote visipowezekana kabisa basi katika ahadi ya Mh Paul makonda, nitagawana nae nusu kwa nusu”>>> Samatta
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Shomari Kapombe aliumia mwishoni mwa mwaka jana akiwa na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Starskatika mazoezi ya mwisho Afrika Kusini kuelekea Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019, toka ameumia Kapombe hajarudi uwanjani rasmi hadi Taifa Stars inacheza na Uganda.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list