Maombi 130 ya walioomba kusamehewa riba ya kodi ya malimbikizo kwa walipa kodi mbalimbali nchini yamekataliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kusamehewa.
Kwa mujibu wa sheria walipakodi hao kwa sasa watatakiwa kulipa kiasi walichokuwa wanadaiwa ikiwamo riba na faini, kwa mujibu wa sheria.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema maombi yaliyowasilishwa ni 9,220 na yaliyokubaliwa ni 6,987, Julai mwaka jana, TRA ilitangaza vigezo sita kwa wanaostahili kupata msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya kodi na kupewa siku 30 za kukamilisha malipo hayo.
Kayombo alisema maombi 2,113 yalikuwa chini ya ukaguzi maalum ili kujiridhisha nayo kabla ya utekelezaji, kutokana na msamaha huo kodi iliyolipwa TRA ni zaidi ya Sh. bilioni 973.4.
Aidha, hadi kufikia Januari 31, mwaka huu riba ya kodi iliyolipwa ni zaidi ya Sh. bilioni 247.5, huku riba na faini iliyopatikana ikiwa ni Sh. bilioni 849.8.
Vigezo sita vilivyotolewa TRA kwa wanaostahili kupata msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya nyuma ya kodi.
Utekelezaji wa msamaha huo ulitokana na maelekezo ya Rais John Magufuli, dhidi ya malalamiko ya wafanyabiashara nchini, katika mkutano wake na Baraza la Taifa la Wafanyabiashara (TNBC), uliofanyika Machi 20, mwaka huu, walilalamikia kuwapo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu.
No comments:
Post a Comment