We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, March 26, 2019

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya, Imependekeza umri wa kufanya ngono uwe ni miaka 16 badala ya 18

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imependekeza umri wa kuruhusiwa kujihusisha na ngono nchini Kenya upunguzwe kwa miaka miwili. Kwa sasa, sheria za Kenya zinaruhusu vijana wa miaka 18 na kuendelea kufanya ngono.
Kwa mujibu wa BBC. Gazeti binafsi la The Standard la nchini Kenya linaripoti kuwa majaji watatu wa mahakama hiyo wapendekeza maboresho ya sheria na umri wa kuruhusiwa kufanya ngono ushushwe kutoka miaka 18 mpaka 16.
Gazeti hilo linadai kuwa majaji hao wanapingana na adhabu kali ya vifungo virefu jela wanayopewa vijana wa kiume kwa “kushiriki ngono na mabinti ambao tayari ama wanataka kuwa wakubwa.”
Majaji hao wametumia mfano wa kesi moja ambayo walitupilia mbali kifungo cha mika 15 alichopatiwa mwanaume mmoja kwa kumtia mimba msichana wa miaka 17.
Pia wanadai kuwa baadhi ya wavulana na wasichana walio chini ya miaka 18 wanajihusisha na mahusiano ya kingono “wakiwa macho meupe kabisa (wakijua wafanyayo),” linaripoti gazeti hilo.



“Magereza yetu yamejawa na vijana wa kiume ambao wanatumikia vifungo virefu kwa kushiriki ngono na wasichana ambao ridhaa yao ya kufanya matendo hayo haitambuliki kisheria sababu tu hawajafikia miaka 18,” majaji hao wamekaririwa wakisema.
“Yawezekana hawajafikia umri wa utu uzima lakini yawezekana tayari wameshafikia umri wa kuridhia kufanya ngono, na wanaweza kuchukua hatua sahihi na za kiweledi kuhusu maisha yao na miili yao.”
Katika kesi husika, Eliud Waweru alifungwa baada kumtia mimba msichana ambaye alikuwa amemaliza kidato cha nne.



Waweru kabla alipatana na baba wa binti huyo kuwa atalipa mahari ya KSh80,000 baada ya kutoroka na mpenzi wake huyo.
Alikamatwa na kufikishwa mahakamani baada yakushindwa kulipa mahari hiyo.
Majaji wamesema kuwa msichana huyo alilazimishwa kutoa ushahidi dhidi ya Waweru na wazazi wake, jambo ambalo aliliandika kwenye barua zake mbili na kutishia kujiua.
Waweru ambaye ametumikia miaka nane ya kifungo hicho ameachiliwa huru Ijumaa iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list