Mtu mmoja amefariki dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya kutokea mapigano baina ya wananchi wa vijiji vya Lendikinya na Emairete wakigombea ardhi kati ya msitu wa hifadhi ya Lendikinya na vijiji hivyo vilivypo katika kata ya Sepeko na Monduli juu, wilayani Monduli mkoani Arusha.
Kufuatia hali hii Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Monduli mkoani Arusha limeazimia kusitisha shughuli zote za kilimo zilizokuwa zikifanyika katika vijijiji vitatu vya Lendikinya, Emairete, na Arkalia kutokana na mgogoro huo na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwaandikia barua wananchi wote wanaojihusisha na shughuli za kilimo kufika ofisini kwake.
Machi 28 majira ya saa kumi na moja jioni kulitokea mapigano katika mpaka wa vijiji hivyo na kusababisha watu sita kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa mapanga, kuchomwa mishale na kupigwa mawe,na kulazwa katika hospitali ya wilaya Monduli ambapo wawili kati yao wakiwa na hali mbaya na kuhamishiwa hospitali ya Mkoa ya Mountmeru ambapo mmoja alipoteza maisha.
No comments:
Post a Comment