Rais John Magufuli amemueleza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simoni Sirro kutosita kuwachukulia hatua watendaji wa jeshi hilo wasiotimiza majukumu yao ipasavyo.
Akizungumza leo Ikulu Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawaziri mawili, Rais Magufuli amemueleza IGP kuwa kama inawezekana kuwepo na utaratibu wa kutoa nyota kama ulivyo wa kuweka.
"Lazima tujenge taswira ya Jeshi la Polisi kama lilivyoasisiwa na Mwalimu Nyerere. Kama kuna maafisa wa Jeshi la Polisi wanaofanya vibaya leta taarifa ili hata nyota zao zipunguzwe na wanaoshindwa wasipelekwe Makao Makuu," amesema Rais Magufuli.
Mawaziri Walioapishwa leo ni Dkt. Agustine Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria ambapo awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, pamoja na Prof. Palamagamba Kabudi Kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambapo awali alikuwa Waziri wa Katibana sheria.

No comments:
Post a Comment