Ukiachia ‘pambano’ kubwa la kesho la Taifa Stars vs Uganda, Tanzania ilikua na pambano jingine kubwa leo huko Nairobi Kenya ikiwakilishwa na Bondia Mtanzania Mtoto wa Tanga Hassan Mwakinyo.
Mwakinyo amemaliza kilichompeleka Kenya kwa kupambana na Bondia wa Argentina Sergio Gonzalez ambapo Mtanzania huyu amechukua ushindi kwa kumpiga Sergio kwa K.O kwenye round ya 5.

Mwakinyo kwenye pambano la leo ( picha kwa hisani ya Super Sport 8)
Baada ya ushindi huo, Mwakinyo amesema “Ushindi wangu wa leo ni maalum kwa Taifa Stars hapo kesho, natamani ushindi huu ukawe mfano kwa Wachezaji wa Stars, nawashukuru Watanzania kwa dua zenu na tusiache kuwapombea Taifa Stars”
Siku moja kabla ya pambano lake Mwakinyo alitumia Instagram yake kuandika “Ndugu zangu wana taifa mko kwenye maombi yangu nawaamini sana na pia naomba nikawe mfano wa kuigwa siku ya kesho, NCHI YETU TIMU YETU TAIFA LETU”
No comments:
Post a Comment