Naibu Kiongozi wa Chama Cha ACT - Wazalendo, Juma Duni Haji, amesema Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa hastahili kulaumiwa kwa uamuzi huo wake wa kurejea CCM.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
Akizungumza siku chache tangu atangaze kuingia ACT - Wazalendo ambapo amesema, “sitaki kuongea mengi juu ya uamuzi huu wa bwana Lowassa, lakini kwa mtazamo wangu najua hakupenda kuchukua uamuzi huu, ila imembidi tu sababu hakuna namna".
“Lowassa ni mtu mzima, anajua ukweli wake na hata CCM wanajua walichomfanyia, nyuma ya uamuzi wake tumesikia misukosuko mingi, kuna mashamba, biashara, mara mkwe, lakini sisi si watoto wadogo, tunafahamu yanayoendelea ila ngoja tunyamaze,” ameongeza Duni.
Mwaka 2015 Juma Duni alikuwa mgombea mwenza wa nafasi ya Urais katika Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambapo mgombea Urais alikuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa lakini baadaye Duni alitangaza kurejea Chama Cha Wananchi CUF.
No comments:
Post a Comment